30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

UHISPANIA: MWANAMKE WA MIAKA 64 AJIFUNGUA MAPACHA

Mwanamke mwenye umri wa miaka 64 amejifungua mapacha wawili ambao ni wa kike na wa kiume katika eneo la Burgos, kaskazini mwa Uhispania.

Mama huyo alijifungua kupitia upasuaji bila matatizo yoyote katika Hospitali ya Recoletas

Taarifa zilizopo zinasema mwanamke huyo ambaye hakutajwa alifanyiwa matibabu ya uzazi nchini Marekani na ndipo alipofanikiwa kubeba ujauzito huo wa mapacha wake.

Pamoja na hilo, mwaka 2012 mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kike ambaye baadaye alichukuliwa na kulewa na huduma za kijamii kwakuwa alionekana kushindwa kumlea.

Hata hivyo Mnamo mwezi Aprili 2016 mwanamke mmoja wa Kihindi aliye na umri wa miaka 70 Dajlinder Kaur , alijifungua mtoto mwenye afya katika jimbo la Haryana nchini India baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kizazi chake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles