26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUKARABATI UWANJA WA NDEGE WA MTWARA JULAI MWAKA HUU

Serikali imesema  ina mpango wa kukarabati uwanja wa ndege wa  Mtwara  ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua uwanjani hapo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema kuwa ukarabati huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege, maeneo ya maegesho pamoja na barabara yenye urefu wa km 1.5 inayoingia katika uwanja huo.

"Tunategemea mwisho wa mwezi huu kutangaza zabuni ya ukarabati wa uwanja huu, matumaini yetu tutampata mkandarasi mzuri kwa ajili ya kazi hii," alisema Waziri Mbarawa.

 Waziri Mbarawa alifafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa  inajenga uzio katika uwanja huo ili kuhakikisha usalama wa uhakika uwanjani hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles