27.7 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

UCHAFU TANDALE WAMCHEFUA LUGOLA

NA ASHA BANI-DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola, jana aligeuka   mbogo na kuwakemea hadharani watendaji wa Manispaa ya Kinondoni  kwa kushindwa kusimamia   usafi katika manispaa hiyo.

Alionyesha hali hiyo Dar es Salaam jana alipokuwa akikagua   usafi katika eneo la Tandale kwa Mtogole.

Waziri aliwataka viongozi wa halmashauri zote nchini wakiwamo wakurugenzi kuhakikisha wanasimamia   usafi vinginevyo watachukuliwa hatua.

Akiwa katika eneo hilo,   Lugola, alianza kwa kusikiliza kero za wananchi kuhusu usafi wa mazingira.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mhalitani, Sudi Makamba, alisema wanakabiliwa na changamoto ya uzoaji taka, licha ya wananchi kuchangia huduma hiyo lakini manispaa haipeki magari  ya kuzoa taka.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli alisema si jukumu lao ila  utaratibu wao ni kuzoa taka za umma hasa katika maeneo ya sokoni na siyo katika nyumba za watu.

“Tatizo lipo kwa viongozi wa serikali za mitaa wakiwamo watendaji na wenyeviti kwa kushindwa kusimamia wakandarasi,” alisema Kagurumjuli

Baada ya utetezi huo mkurugenzi, Lugola alisema  ameamua kufanya operesheni hiyo kutokana na nchi kukumbwa na athari ya mabadiliko ya   tabianchi, uchafuzi wa hali ya hewa.

Alisema kwa sasa katika  Bahari ya Hindi,  hasa katika mikoa ya Tanga, Pwani Lindi na Mtwara, maji yameongezeka na kuathiri kingo za bahari hali inayosababishwa na mmomonyoko wa udongo.

Alisema hali hiyo inachangiwa na shughuli za binadamu ikiwamo uchafuzi wa mazingira na uzalishaji wa taka ngumu kama vile mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles