23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

WAIRANI 10 KORTINI KWA KUSAFIRISHA HEROIN

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

SERIKALI imewafikisha mahakamani raia 10 wa Iran na Watanzania wawili wakikabiliwa na mashtaka  matatu ya kusafirisha dawa mbalimbali  za madawa ya kulevya zikiwamo kilo 111.02 za heroin.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana   mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alidai  kwamba washtakiwa walikutwa katika Ukanda wa Bahari ya Hindi upande wa Tanzania.

Washtakiwa ni Nabibakshsh Bibarde, Mohammed Dorzade, Abdallah Sahib, Ubeidulla Abdi, Naim Ishaqa, Moslem Amiree, Rashid Badfar, Omary Ayoub, Tahir Mubarak, Abdulmajid Asqan, Ally Abdallah na Juma Juma.

Kishenyi alidai  Oktoba 25, mwaka huu  katika ukanda huo wa Bahari ya Hindi upande wa Tanzania, washtakiwa walisafirisha kilo 111.02 za heroin.

Inadaiwa  siku hiyo hiyo washtakiwa hao pia walikutwa wakisafirisha  gramu 235.78 za   bangi.

Kishenyi alidai   siku hiyo washtakiwa hao walisafirisha mchanganyiko wa   bangi na kuberi zenye uzito wa kilo 3.34.

Washtakiwa walikuwa wakitafsiriwa lugha ya Kiswahili kwenda Kiirani na mkalimani Meja Ndakeye (45).

Baada ya kusomewa mashtaka hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Upande wa Mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na washtakiwa walipelekwa rumande hadi Novemba 13, 2017 kesi yao  itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles