24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

TuneCore yatua kwa kishindo Afrika Mashariki

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI inayoongoza katika usambazaji muziki kidigitali na kukusanya mirabaha ya wasanii huru, TuneCore, imezindua rasmi shughuli zake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Jade Leaf ameajiriwa kama Mkuu wa TuneCore Afrika ya Kusini na atashiriki majukumu kwenye nchi za Afrika Mashariki huku Chioma Onuchukwu atashughulika na TuneCore upande wa Afrika Magharibi.

Leaf na Chioma wataripoti kwa Faryal Khan-Thompson ambaye ni Makamu wa Rais wa Kimataifa wa jukwaa hilo muziki kwa muziki wa Afrika.

Chioma atakuwa Nigeria na atasimamia nchi zilizopo Afrika Magharibi ikiwemo Ghana, Liberia, Sierra Leon na Gambia akisimamia pia Tanzania na Ethiopia.

Himaya ya Leaf inajumuisha Afrika ya Kusini ikiwemo Afrika Kusini yenyewe ambayo ni makao makuu ya TuneCode pia Namibia, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi na Lesotho pamoja na Kenya na Uganda.

“Ninafuraha kuwa ninajiunga na kampuni huru maarufu ya usambazaji wa muziki, hasa katika karne hii ya ajabu sana kwa wabunifu wa muziki barani Afrika wakati ambao tunapata kutambuliwa kimataifa na tunaongezea bidii.
“Ninatazamia kushirikiana na kuwaunga mkono wasanii wa nchi hizi ninazozisimamia,” amesema Chioma.

Kabla ya kujiunga na TuneCore, Chioma alikuwa Meneja Masoko katika kampuni ya uduX Music, jukwaa la kutiririsha muziki nchini Nigeria.

Hapo alifanya kazi moja kwa moja na wasanii maarufu wa Afrika kama vile Davido, Yemi Alade, Patoranking, Kizz Daniel na wengine wengi.

“Ninafuraha sana kujiunga na timu hii wakati ambao mazungumzo ya kimataifa yanahusu uhuru na umiliki,” amesema Leaf.

Awali, Leaf alifanya kazi katika kampuni kubwa zaidi Afrika ya TV ya kulipia, Multichoice kama Meneja wa Masoko wa Vituo vya Vijana na Muziki, ambapo aliongoza katika kukipa sura mpya kituo kikubwa cha muziki Channel O.

Kabla ya hapo alifanya kazi Sony Music Entertainment Africa, akilenga wasanii na maudhui ya Kiafrika, na hata kampeni nyingi za masoko na miradi ya wasanii wa nchini na wa kimataifa.

Katika mwaka wa 2020, TuneCore ilishuhudia ongezeko katika matoleo ya muziki kimataifa, huku wasanii wengi wa Kiafrika wakichagua kutumia wasambazaji wa DIY – DJ Spinall na Small Doctor nchini Nigeria, Spoegwolf nchini Afrika Kusini, Mpho Sebina nchini Botswana na Fena Gitu nchini Kenya.

“Afrika ni soko linalosisimua sana la muziki lenye uwezo mkubwa wa kukua,” amesema Khan-Thompson.

TuneCore, inayomilikiwa na Believe ya Paris, imekuwa ikipanua kwa haraka shughuli zake za kimataifa, kuanzia nchi tano mwaka wa 2020 hadi nchi nane na maeneo matatu makuu katika mwaka 2021.

Kampuni hii iliongezea India, Urusi na Brazili mwaka uliopita na mwaka huu ikaongezea LATAM, Asia ya Kusini Mashariki na Afrika huku ikutumia lugha 13 na zinaendelea kukua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles