Paris, Ufaransa
Mwanamuziki anayekuja kwa kasi kutoka nchini Ufaransa, Desclo James, ameendelea kuwapa raha mashabiki wa dansi na wimbo wake, Pasola Mbese’ aliomshirikisha msanii wa Cameroon, SMELO.
Desclo, amesema wimbo wenye mahadhi ya sebene umebeba ujumbe wa kutumia kilicho chako kwa starehe zako bila kujali watu watasema nini.
“Wimbo huo ni juu ya kutumia kile chako bila kujali watu wanafikiria nini kuhusu wewe, kama nina pesa yangu ninachofanya chocjote ni biashara yangu haikuhusu. Pia Mbese maana yake ni samaki nasema kata samaki kila mtu ale upande wake ndio maisha yalivyo, video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” amesema Desclo mwenye asili ya Kongo DRC.