25.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

‘TUMIENI NJIA ZA MILA KUWAKABILI TEMBO’

 

Na Derick Milton


MBUNGE wa   Itilima mkoani Simiyu, Njalu Slanga, amewaomba wazee wa  mila katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa kutumia njia za  mila katika kupambana na tembo wanaotoka katika pori hilo.

Slanga alisema  zamani wazee wa  mila walikuwa wakitumia njia hizo  kupambana na wanyama hao wanapovamia   mazao   na nyumba zao,  bila  a kuwapo madhara kati yao na wanyama hao.

Mbunge huyo alikuwa alitoa kauli hiyo   katika Kata ya Logalombogo  baada ya wananchi  kumweleza kuwa tembo wamekuwa kero kubwa kwao na familia zao.

Walisema  wamekuwa wakilazimika kulala mapema kwa kuogopa kukutana na wanayama hao na kusababisha kuishi kwa hofu kila siku.

“Tembo hawa wamesababisha sisi kuishi kwa hofu, kila mwaka kwetu ni njaa kutokana na mazao yetu kuharibiwa na wananayama hawa.

“Hiki kilimo kimekuwa cha muda mrefu,  sijui mnataka na sisi tuchukue uamuzi mgumu?” alisema Maria Manyangu.

Mbunge huyo aliwataka wananchi hao wasichukue uamuzi wa kuwaua tembo hao.

Aliwaomba wazee   kutumia njia za mila kuzuia wanyama hao wasifanye uharibifu huo.

Vilevile alisema atalifanyia kazi tatizo la wanyama hao   kwa kuomba kijengwe  kituo cha askari wa wanayama pori katika vijiji vilivyoko kwenye kata hiyo  kuzuia maafa yanayosababishwa na wanyama hao.

“Wakati mimi naendelea kupambana kuletwa   vituo vya askari kwenye kata hii, wazee nawaomba tutumie zile njia za zamani, mbona uko nyuma tulikuwa tunafanikiwa na hawa wanyama wanarudi kwenye pori?

“Hakuna madhara kwetu hata kwa wanyama wenyewe,” alisema Njalu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles