25.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 14, 2024

Contact us: [email protected]

LEMA, NASSARI KUWASILISHA USHAHIDI TAKUKURU

Na JANETH MUSHI-ARUSHA


WABUNGE wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki),wanatarajia kuwasilisha ushahidi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu kutuhumiwa kupokea rushwa.

Hatua hiyo, inakuja zikiwa zimepita siku tano tangu wabunge hao walipodai madiwani hao walihama kuunga mkono rushwa na si kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kama walivyodai.

Lema jana aliliambia MTANZANIA kuwa tayari wamezungumza na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe ambapo alitoa maelekezo kwao kupeleka ushahidi huo Takukuru.

“Nassari anakuja kesho kutwa (kesho), kutoka Nairobi, amezungumza na Mbowe ambapo alitoa maelekezo, hivyo Nassari akija nchini tutapanga kwenda kumwona Mkurugenzi wa Takukuru,” alisema Lema.

Jumapili wiki hii, Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa anaoushahidi usiokuwa na shaka kuhusu madiwani wa Chadema waliohamia CCM kuhongwa.

Kutokana na hilo, Nassari alisema endapo ushahidi huo hautakuwa wa kweli atajiuzulu ubunge wake.

Pia alisema yupo tayari kukutana kukutana na Rais, Mkurugenzi wa Takukuru, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai(DCI),Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,kuwaonyesha ushahidi usiotia shaka na kwamba baada ya siku 14 asipoitwa kuonyesha ushahidi huo atauweka hadharani.

Hadi sasa madiwani tisa wa Chadema wamejiuzulu na kuhamia CCM ambapo kati ya hao, watano wanatoka Jimbo la Arumeru Mashariki,Arusha Mjini wawili,Monduli mmoja na Longido mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles