24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP, JESHI LIKO TAYARI KUIKABILI KOREA KASKAZINI

 

NEW YORK, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema jeshi la Marekani liko tayari kukabiliana na Korea Kaskazini wakati wowote ule.

“Suluhu ya kijeshi sasa ipo, imepangwa na iko tayari, Korea Kaskazini wakithubutu kuchukua hatua isiyo ya busara. Twatumai Kim Jong-un atachagua njia nyingine!” Trump ameandika kwenye Twitter.

Amesema hayo huku Korea Kaskazini ikimtuhumu kwa kukaribia kutumbukiza rasi ya Korea katika vita ya nyuklia.

Serikali ya Korea Kaskazini inakamilisha kuandaa mpango wake wa kurusha makombora karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.

Idara ya mambo ya nje katika kisiwa hicho katika bahari ya Pasifiki imetoa mwongozo pamoja na ushauri kwa wakazi wa kisiwa hicho kuhusu jinsi ya kujiandaa kukiwa na tishio la makombora.

Aidha, Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) jana liliituhumu Marekani kwa “jaribio la kihalifu la kusababisha mkasa wa kinyukilia katika taifa hilo la rasi ya Korea.”

Shirika hilo lilisema Marekani inafanya kila juhudi kufanyia majaribio silaha zake za nyuklia katika rasi ya Korea.

Awali, alikuwa ameitahadharisha Korea Kaskazini kwamba inafaa kuwa na “wasiwasi sana” iwapo itatenda lolote kwa Marekani.

Alisema utawala wa taifa hilo utakuwa shida kubwa “ambayo ni mataifa machache sana yaliyowahi kukumbana nayo” iwapo “hawatabadilika”.

Kadhalika Trump alikuwa awali ameshutumu serikali za awali za Marekani, akisema zilionyesha udhaifu sana zikikabiliana na Korea Kaskazini na pia akashutumu mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini, akisema kwamba inafaa “kufanya juhudi zaidi.”

Alisema: “Nawaambia, iwapo Korea Kaskazini itafanya jambo lolote hata kwa kufikiria tu kuhusu kumshambulia mtu tunayempenda au tunayewakilisha au washirika wetu au sisi wenyewe inaweza kuwa na wasiwasi sana, sana.”

“Nitawaambia ni kwa nini…ni kwa sababu mambo yatawatendekea ambayo hawajawahi kufikiria kwamba yanaweza kutokea.”

Aliongeza: “Nawaambia hivi, Korea Kaskazini inafaa kujiweka sawa au wataona shida kubwa kiasi ambacho ni nchi chache sana zilizowahi kushuhudia.”

Korea Kaskazini ilisema Jumatano kwamba inapanga kurusha makombora ya masafa ya wastani na ya masafa marefu kuelekea kisiwa cha Guam, ambapo kuna kambi ya ndege za kivita za kuangusha mabomu za Marekani.

Hata hivyo, kufikia sasa hakujakuwa na dalili zozote kwamba huenda kisiwa hicho cha Guam kikashambuliwa. Korea Kaskazini ilikuwa imeghadhabishwa na vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa.

Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.

KCNA imesema Korea Kaskazini, ambayo imefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano, itajibu vikali na kwamba “Marekani italipia” kwa kuchangia kutunga vikwazo hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles