TRUMP AIAHIDI PALESTINA AMANI

0
433

RAMALLAH, UKINGO WA MAGHARIBI


RAIS Donald Trump wa Marekani, amesema atafanya kila awezalo kuzisaidia Israel na Palestina kupata amani.

Katika mazungumzo na Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas juzi, alimshukuru kwa kuwajibika kuchukua hatua zinazohitajika kupambana na ugaidi.

Israel na Palestina hazijafanya mazungumzo kwa miaka mitatu, na Trump anakiri kuwa itakuwa mojawapo ya makubaliano magumu kusimamia kufikiwa.

Trump ambaye alitembelea Saudi Arabia, Israel na maeneo ya Palestina, alimaliza ziara yake hiyo ya Mashariki ya Kati jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here