28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

JAMMEH ADAIWA KUIBA DOLA MILIONI 50, MALI ZAZUIWA

BANJUL, GAMBIA


ALIYEKUWA Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, aliiba kiasi cha dola milioni 50 za taifa hilo kabla kukimbilia uhamishoni nchini Guinea ya Ikweta, Januari mwaka huu baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miaka 22.

Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Sheria wa Gambia, Abubacarr Tambadou, aliyesema Jammeh binafsi aliamuru fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Gambia na Benki ya Gamtel kati ya mwaka 2013 na 2017.

Waziri huyo aidha alisema kuwa wamepata kibali cha mahakama kuzifungia au kuzizuia kwa muda mali zinazofahamika kumilikiwa na Jammeh na kampuni zinazohusishwa moja kwa moja na kiongozi huyo.

Waziri Tambadou alisema amri ya mahakama iliyotolewa juzi inalenga kumzuia Jammeh kuziuza mali zake na amethibitisha amri hiyo inahusu mali za kiongozi huyo zilizopo Gambia pekee.

Jammeh anayelaumiwa kwa kuiba pesa hizo kupitia kampuni ya Serikali ya mawasiliano, alishindwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Desemba mwaka jana.

Alikubali kuondoka madarakani baada ya vikosi vya ukanda wa magharibi mwa Afrika kutishia kumwondoa kwa nguvu.

Magari ya kifahari na bidhaa nyingine ziliripotiwa kuingizwa katika ndege ya mizgo ya Chad wakati Jammeh alipokuwa akiondoka nchini humo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles