29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

TPA yakiri kuwapo kwa usumbufu bandarini wakati wa kutoa mizigo

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) imekiri kuwa bado kuna malalamiko yanayotokana na usumbufu kwa wateja wao wakati wa kuchukua au kusafirisha mizigo kutoka kwa baadhi ya vitengo vyao.

Kauli hiyo imetolewa Jumamosi Agost 13, 2022 na Mkurugenzi wa Mipango, Ubora na Udhibiti Vitaharishi, Dk. Boniface Nobeji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuli za bandari kwa mwaka 2020/21 na mwelekeo wao kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Dk. Nobeji amesema siyo kila lalamiko linasababishwa na watendaji au watumishi wa mamlaka hiyo bali kuna taasisi zingine na wakati mwingine wateja wenyewe kwa kutokukamilisha baadhi ya nyaraka ili mtu aweze kuchukua mzigo wake.

Dk. Nobeji amesema Mamlaka hiyo ina mtandao mpana na ndani yake kuna taasisi 34 hivyo wanabeba changamoto nyingi za wadau kwa hiyo kuna baadhi ya maeneo yawezekana kuwa wao lakini pengine kuna haja ya kuangalia na upande wa wanaohudumiwa.

“Hilo la malalamiko hatukatai, lakini linapaswa kuangaliwa na upande wa pili kwa tunaowahudumia nao kuona kuna nini,wakati mwingine sisi tunatimiza wajibu wetu lakini mtu anakuja hana nyaraka na mzigo umeshakaa siku nyingi kwa hiyo lazima tujiridhishe kwanza,” amesema Dk. Nobeji.

Kuhusu mafanikio ametaja kuwa, kwa mara ya kwanza katika mwaka wa fedha uliopita TPA imefanikiwa kukusanya Sh trilioni 1 licha ya muda mrefu kuwa na lengo hilo lakini hawakufikia na kwa mwaka huu wa fedha wanalenga kukusanya Sh trilioni 1.2.

Pia, wamefanikiwa kuwa na ulinzi na usimamizi mzuri wa mizigo ya wateja wao kutoka nchi tano ambazo zinahudumia na bandari za Tanzania huku akieleza kuwa wamerasimisha bandari 20 katika maeneo mbalimbali ambapo sasa zinachangia kwenye usafirishaji wa mizigo kwa halali.

Ametaja kwa mwaka uliopita walitoa huduma ya mizigo kwa tani milioni 20, makasha 823,000, shehena ya magari ilifikia 203,932 ikiwemo meli kubwa ya magari iliyokuwa na magari zaidi ya 4,000 lakini akazitaja bandari za Mtwara na Mwanza kwamba zimekuwa zikifanya vizuri na kuongeza shehena za mizigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles