22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

DAWASA kuanza ujenzi wa Bwawa la Kidunda Oktoba mwaka huu

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)imesema ujenzi wa Bwawa la Kidunda utaanza rasmi Oktoba, mwaka huu ili kufikia malengo ya utoaji huduma kwa asilimia 100 ambapo zaidi ya Sh bilioni 378 zitatumika.

Hayo yameelezwa jAgosti 13, 2022 ijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi na utoaji huduma kwa maeneo yanayohudumiwa na mamlaka hiyo kwa mwaka 2021/22 na mipango ya 2022/23.

Luhemeja amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaama na sehemu ya mkoa wa Pwani watakuwa wakipata maji kwa asilimia 100 huku maeneo mengine yakitarajia kukamilishwa mapema mwakani.

Mtendaji huyo ameelezea mkakati huo kuwa unakwenda sambamba na kuongeza mtandao wa huduma ya maji taka ambapo wametenga zaidi ya Sh bilioni 19 kwa huduma hiyo na kutawanya mabomba katika vijiji 74.

Amesema mkakati mwingine ni kuendelea kuongeza mtandao wa maji katika maeneo mengi ili kukidhi malengo kwani inakadiliwa kuwa ifikapo 2025 jiji hilo kubwa la kibiashara litahitaji Lita milioni 740 kwa matumizi ya wananchi wake.

Amesema kati ya majimbo 16 yanayohudumiwa na Dawasa ni jimbo la Ukonga na Kibamba ambayo huduma hiyo bado iko nyuma kiasi ukilinganisha na maeneo mengine na kwamba kuna baadhi ya maeneo wanapata maji kwa asilimia 100.

Kwa sasa mamlaka hiyo imetaja kuwa inatoa huduma kwa asilimia 96 ya malengo ambayo ni Lita 520 milioni wakati mahitaji kamili ya maji kwa jiji hilo ni lita milioni 544, hivyo wanaupungukiwa wa lita milioni 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles