23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Vigezo vitatu vyatumika kutoa ruzuku kwa Asasi za Kiraia

Ramadhan Hassan,Dodoma

VIGEZO vitatu vimetumika kutoa ruzuku ya Sh bilioni 4 kwa Asasi za Kiraia 89 kati ya 1,200 zilizoomba huku Shirika la Foundation For Civil Society (FCS) likidai limeweka mfumo madhubuti wa kudhibiti kila shilingi jinsi itakavyotumika.

FCS imesema taasisi zisipofuata utaratibu watachukua hatua kali lengo likiwa ni kuhakikisha fedha hizo zinawahudumia wananchi.

Hayo yameelezwa leo Agosti 15, jijini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga wakati akizungumza kwenye warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI 89   zilizochaguliwa kupata ruzuku.

Kiwanga amevitaja vigezo vilivyotumika ni  pamoja na kuwa na mifumo ya kuthibiti fedha hizo,wakaguzi kuangalia kama taasisi hizo zipo hai,pamoja na maombi waliyotuma.

“Huu mchakato haukuwa ni wa upendeleo labda kuna mjomba pale Foundation hapana ulikuwa ni mchakato ‘very independent’ na ulishirikisha wadau ndani wa ndani na na napenda kuwahakikishia hao waliopata ni best,” amesema Kiwanga.

Amesema FCS imeweka mfumo madhubuti wa kuhakikisha  kila Sh inatumika kwa lengo lilokusudiwa huku  taasisi zizofuata utaratibu watachukua hatua kali.       

Amesema taasisi 1,200 ziliomba kupata fedha hizo za ruzuku lakini zilizokuwa na vigezo ni 89 huku asilimia 70 ni mpya.

Mkurugenzi huyo amesema kiasi hicho cha fedha kitatumika kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya programu za utawala bora katika sekta za maji.

Pia katika sekta za  elimu, afya na kilimo, usawa wa kijinsia, ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.

Kiwanga amesema FCS imejitika katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.

“FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao,” amesema Kiwanga.

Kiwanga amesema  kuwa kumekuwepo ongezeko la migogoro katika rasilimali hivyo kwa sasa kuna taasisi 10 zitafanya kazi ya kuitatua hususani maeneo ya Kusini, Morogoro na Kilosa.

Naye, Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo amesema FCS wanafanya kazi na mashirikia madogo  ambao  ni wabia na viongozi wa klasta za programu wambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa.

Amesema wanafanya kazi na asasi za kijiji, kata na wilayani huku wabia ni mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu.

Chilimo amesema  mashirika yanayofadhiliwa na FCS sio waruzukiwa tu, ni wabia pia na kwamba baadhi ya misingi ya ubia ni uelewa wa pamoja,malengo ya pamoja, na kuaminiana ili kuweza kufikia malengo ya pamoja.

“Tumekuwa walezi wa sekta ya AZAKI, tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa,”amesema Chilimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Women For Self Innitiative wilaya ya Mkinga mkoani Tanga (TAWSEA), Bernadetha Choma alisema wao kama NGO’S kupitia ruzuku wanazopewa zitaenda kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles