30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Timu ya dharura kukabili corona yafundwa

MWANDISHI WETU – DODOMA

DHANA ya afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za afya katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomwathiri binadamu, imeendelea kufundishwa kwa wataalamu wa sekta ya afya, kilimo na mifugo, huku wakitakiwa kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya binadamu na wanyama ambayo hutokea mara kwa mara.

Akizungumza jana wakati wa kufungua mafunzo hayo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, alisema kuwa ushirikiano wa wataalamu na sekta za afya kwa kutumia dhana ya afya moja hivi sasa ni ajenda ya dunia.

Alisema kuwa dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani ambako mwingiliano huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi, utandawazi, ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.

“Mafunzo haya ni muhimu sana nchini kwa kujenga uwezo wa nchi katika utayari wa kukabiliana na magonjwa yanayosambazwa na wanyama na kuathiri wanyama na binadamu.

“Tanzania tumeambiwa yupo mgonjwa wa corona19, ambapo tumeambiwa mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu na Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae nchini,” alisema Kanali Matamwe.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Ndaki ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Amandus Muhairwa, alisema kuwa sekta za afya zikishirikiana katika kudhibiti magojwa, zitasaidia kuimarisha afya ya binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukua tahadhari kwa wakati.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles