25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mbatia awataka wananchi kuchukua tahadhari corona

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amesema Watanzania wanatakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa corona kwa kutumia vifaa maalumu vya kujikinga ili kuzuia usiendelee kuenea na kuleta maafa zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mbatia alisema kuwa watu wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa kujikinga zaidi kwa sababu ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba.

Alisema Watanzania wanatakiwa kuwa kitu kimoja kushirikiana bega kwa bega katika kukabiliana na changamoto hii.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuwa watu wanatakiwa wasiwe na hofu na shaka kwani hofu ni hatari katika mwili wa mwanadamu.

Amewaasa wananchi kuchukua taarifa sahihi kuhusu ugonjwa wa corona na hatua stahiki na kupambana na janga hili.

“Mamlaka husika ikiwemo kitengo cha majanga ishughulikie suala hili kwa kuhakikisha wananchi wanapata vifaa vya kujikinga na ugonjwa huu, pia wapate taarifa sahihi ya mara kwa mara ili kuondoa hofu na migongano inayoweza kujitokeza,” alisema Mbatia.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles