21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

TASAF YAWAPIGA MSASA WATAALAMU LINDI

Hadija Omary, Lindi

Wataalamu mbalimbali 30 kutoka ngazi ya kata na vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, wamepatiwa mafunzo ya stadi za maisha kwenye programu ya kukuza uchumi wa kaya za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini yanayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Ofisa Mafunzo wa Tasaf, Katherin Kisanga amewataja wataalamu hao wanaopatiwa mafunzo kuwa ni maofisa ugani, maofisa mifugo na uvuvi, maenedeleo ya jamii  na maofisa afya kutoka katika ngazi ya kata na vijiji ambao watakuwa wawezeshaji katika ngazi ya eneo la utekelezaji kuhusu mafunzo ya stadi za maisha kwa walengwa wa kaya masikini.

Akizungumza na washiriki wa  mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Mratibu wa TASAF Wilaya ya Lindi, Christian Amani amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utaratibu wa kutekeleza shughuli za kukuza uchumi wa kaya za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa katika awamu ya tatu ya TASAF.

“Uanzishwaji wa programu hiyo ya kukuza uchumi wa kaya unahusu utekelezaji wa shughuli mbali mbali zitakazo saidia ukuaji wa uchumi wa kaya na walengwa kufanya shughuli zao ambazo zitapanua uchumi wao.

“Shughuli hizo ni pamoja na kuwapatia stadi za maisha, ikiwa imelenga kutoa mafunzo juu ya ujasiliamali, namna ya kubuni wazo la biashara, namna ya kufanya biashara na aina ya biashara anayotakiwa kufanya ambapo walegwa wanatarajia kupata ujuzi utakaowasaidia kufanya biashara zao kwa faida endelevu, kupata kipato na kupunguza umasikini,” amesema.

Amani  aliwataka wakufunzi hao kuwaelimisha walengwa wa mpango huo wa kunusuru kaya maskini kuhusu hatua zinazotakiwa kufuatwa, huku akiahidi timu ya wataalamu kutoka TASAF Makao Makuu wakishirikiana na wawezeshaji wa kitaifa kufanya mawasilisho ya mada mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles