24.8 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

TASAF yapiga marufuku walengwa kuchukuliwa fedha

Na DERICK MILTON


MFUKO wa Mandeleo ya Jamii (TASAF)   umepiga marufuku utaratibu wa walengwawa mpango wa kunusuru kaya maskini kuchukuliwa fedha  zao   wanaposhindwa kuhudhuria kwenye   uhawilishaji.

Ilielezwa kuwa umekuwapo   utaratibu wa baadhi ya walengwa katika mpango huo wanaposhindwa kuhudhuri kwenye   uhawilishaji fedha huwatuma ndugu au jamaa zao   kuwawakilisha.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Uhawilishaji wa Mfuko huo, Dorothy Shiyo, akimwakilisha Mkurugenzi wa TASAF, Ladislaus Mwamanga, katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kutembelea walengwa katika Wilaya ya Maswa.

Shiyo aliwataka wasimamizi wa mpango huo wa halmashauri zote nchini kutoruhusu walengwa kutuma wawakilishi wakati wa hatua hiyo, badala yake watumie njia mbalimbali kuhakikisha mlengwa mwenyewe anachukua stahiki zake.

“Huu utaratibu ni marufuku kuendelea kuutumia, hakuna kama mlengwa anaumwa, wahusika wa utoaji hizo fedha mnatakiwa kuhakikisha mnamtafuta huyo mlengwa popote alipo na kumpatia mwenyewe na siyo kuwapatia wawakilishi wake,” alisema Shiyo.

Akizungumzia mpango huo kwenye Wilaya ya Maswa, Shiyo alisema   imepiga hatua kubwa na kutekeleza kwa ufasaha mpango huo kutokana na walengwa wengi kujikwamua katika maisha.

“Tumeona walengwa wengi wamejenga nyumba kubwa, wamefuga, wameanzisha biashara, vikundi vya kukopeshana, hili jambo ni kubwa   na ni mabadiliko mazuri, Maswa mmepiga hatua kubwa,” aliongeza Shiyo.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo, Mratibu wa TASAF Wilaya ya Maswa, Grace Tungaraza alisema  mpango huo umesaidia kwa kiasi kukubwa kupunguza kiwango cha umaskini kilichokuwepo kwa walengwa.

Hata hivyo baadhi ya walengwa waliotembelewa walisema  mpango huo umewasaidia   kujikwamua maisha ikiwamo kujenga nyumba imara, kuanzisha biashara   na kujiongezea kipato kupitia ufugaji.

“Mimi nilikuwa sina hata nyumba, nilikuwa ni mtu wa kutangatanga hapa kijijini, lakini huwezi kuamini leo namiliki nyumba kubwa, mbuzi zaidia ya sita, nimeanzisha biashara lakini najihusisha sana na kilimo,” alisema Naumi Machibya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles