22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Tanesco, Symbion washinda kesi Mahakama Kuu

tanescoNa Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Dubai firm Rental Services &Solutions (RSS), dhidi ya Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya
Symbion Power Tanzania.

Hukumu ya kesi hiyo iliyochukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya nchini, imetolewa na Mahakama Kuu Ijumaa iliyopita.

Akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu  mwishoni mwa wiki, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Symbion anayehusika na masuala ya umma na mawasiliano, Adi Raval, alisema uamuzi huo wa Mahakama Kuu umezidi kuongeza uzito kwenye msimamo wa muda mrefu wa Kampuni ya Symbion kwamba haya madai hayakuwa ya msingi.”
“Tumefurahishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu, kama tulivyoeleza tangu wakati ule, hii ilikuwa ni kesi ya kizushi iliyolenga kuidhalilisha kampuni ya Symbion na Tanesco.

Kesi ilikuwa na madai kadha wa kadha yasiyo na mashiko na yaliletwa na kampuni ambayo ilifanya kazi nchini Tanzania kinyume na taratibu kwa takribani miaka mitatu na kuinyima Serikali ya Tanzania kiasi kikubwa ya fedha za Kodi ya Mapato ambayo kimsingi inahitajika sana.

Kwa mujibu wa Raval, Symbioni walishtuka kusikia mkandarasi aliyekaimishwa kazi hakuwa na biashara iliyosajiliwa wala hakulipa kodi ya asilimia 30 kwa kampuni kama yafanyavyo mengine Tanzania.

Alisema Kampuni ya Symbion Tanzania iliilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kiasi cha Dola za Marekani 50 kama kodi.

Raval aliongeza: “Mbinu ya RSS ilikuwa ni kufungua kesi mahakamani na kuifanya itangazwe kwenye magazeti mengi kadri iwezekanavyo kwa lengo la kuharibu sifa ya Tanesco na Symbion.

Aidha, msemaji huyo wa Symbion alisema watahakikisha wanatumia nguvu zote kuwafuatilia RSS ili waweze kulipa gharama za msingi na hasara walizozipata wakati wa kesi hiyo.

April mwaka huu, Kampuni ya Rental Services and Solutionss ya Dubai ilifungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Symbion na Tanesco akidai wameshindwa kulipa deni lake, kiasi cha dola za Marekani milioni 28, ikiwa ni malipo ya kukodisha mitambo na vifaa vyake katika miradi ya umeme iliyokuwa inatekelezwa na Symbion katika maeneo mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles