31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Benki ABC kutoa mikopo ndani ya saa 48

ABCNa Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

BENKI ya ABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkopo rahisi’.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Easy Banking, Thomson Mwasikili, alisema wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serikalini ili kuhakikisha wanapata huduma hiyo kwa haraka.

“Kwa kupitia huduma hii, tutahakikisha wateja wetu wanapata mikopo yao ndani ya saa 48 kuanzia muda uliowasilishwa. Tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema.

Mwasikili alisema benki yao inatoa mikopo hadi Sh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.

“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka sita na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa mwombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa meneja huyo, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha ambayo ni tofauti na mikopo mingine, kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi.

Pia alisema waombaji watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani Benki ya ABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.

“Endapo mwombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Sh 500,000 zitatolewa kugharamia mazishi. Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti katika benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkopo rahisi kwani hii ndiyo benki pekee inayokusogeza karibu na ndoto zako,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles