30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Tanesco Ilala yawanyooshea kidole wanaowahujumu

Na Asha Bàni -Dar es salaam

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Ilala inatoa rai kwa wananchi wanaohujumu shirika hilo kwa kujiunganishia umeme kwa kutumia vishoka ili kukwepa ulipaji kwenye mita kuacha mara moja.

Tanesco ilala  imefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi ya kampuni ya Wakala wa  usafirishaji abiria kwa ndege ( Cosmos Travel Agency) na kubaini kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi iliyofanywa na kampuni hiyo.

Msimamizi wa Kitengo cha kudhibiti  Mapato wa shirika hilo Wilaya ya Ilala,Bernad Mshilimu akiwa eneo la Mbuyuni Posta alifanya ziara na ukaguzi wa kushtukiza na kubaini mteja kajiunganishia umeme moja kwa moja kutoka Tanesco bila kupita kwenye mita ya Luku  kinyume na utaratibu.

Aliongeza kuwa kitendo hiko kinawanyima mapato shirika yake na kudhorotesha Huduma katika baadhi ya maeneo.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Ilala Deusdedit Hokororo alisema hiyo ni kawaida kwa shirika kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wahujumu wa shirika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Hokororo aliwataka mmwananchiwengine wanapopata taarifa za wizi wa umeme au hujuma kutoa tariarifa kwao ili waweze kulishughulikia na kuwabaini.

“Wananchi wema watakaotoa tarifa hizo watalindwa na itakua siri kati yao na Tanesco ,lengo watu wasilihujumu shirika kwa kuwa linategemewa nchi nzima na umuhimu mkubwa,”alisema Hokororo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles