31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Takukuru yamfikiksha mtumishi NMB Kizimbani

FLORENCE SANAWA-MTWARA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa mtwara imemfikisha mahakamani mtumishi wa benki ya NMB Tawi la nanyumbu Augustino Nziku ambayo ni mdhibiti ubora wa huduma wa banki ya Nmb wilayani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Takukuru mkoa wa mtwara Stephen mafipa amesema kuwa nziku anakabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha shilingi 5,620,500/-kupitia akaunti ya Benki yenye jina la mtoto wake.

Amesema kuwa mshitakiwa huyo atashitakiwa kwa kosa la kusaidia kutendeka kwa kosa kinyume cha kinyume cha kifungu cha 30 cha kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11/2007 ikisomwa pamoja na afya ya 21 ya jedwali la kwanza vifungu vya 57 (1) na 60 (2) vya sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200.

Amesema kuwa kosa hilo alilifanya akishirikiana na juma mbeve katibu mkuu na pacho amcos amabapo yenye atashitakiwa kwa kosa la utakatishaji fedha haramu Na. 12 ya mwaka 2006.

“Unajua wote kwa pamoja watashitakiwa kwa Makosa ya kula njama na kitendo makosa kwakutukumia nyaraka zenye maelezo ya uongo kwa kumdanganya mwajiri kinyume cha sheria ya takukuru”

Inadaiwa kwamba Katika mchakato wa malipo ya wakulima wa zao la korosho msimu wa 2017/18 katika chama cha msingi cha ushirika (AMCOS)  kilichopo wilayani Nanyumbu watu walitenda makosa kwa kuingiza kwenye orodha ya walipwaji jina la mtoto wa mtuhumiwa Augustino nziku kuonyesha kwamba mtoto huyo alistahili kulipwa ilihali hakuuza korosho kitendo ambacho kilimuwezesha mtuhumiwa kujipatia shilingi 5,620,500/-

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles