27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Takukuru Kakonko yaokoa fedha za mwalimu mstaafu aliyetapeliwa

 MWANDISHI WETU-KIGOMA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, imefanikiwa kurudisha Sh milioni 54 za mwalimu mstaafu alizokuwa amedhurumiwa na mkopesha riba miaka sita iliyopita. Kamanda wa Taasisi hiyo wilayani hapa,Ladislaus Ibrahim aliliambia gazeti hili, kuwa aliyeibiwa ni Evodia Pius aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Kasanda, baada ya kukabidhi kadi ya benki kwa mkopesha riba aliyeamua kuhamisha fedha hizo 

Alisema Evodia alistaafu kazi mwaka 2014 na kupewa pensheni ya Sh milioni 70,baada ya kustaafu alidanganywa na mkopesha riba ambaye hakutajwa jina lake alimkopesha Sh milioni saba ili kujenga nyumba, kisha akamuibia mama huyo kiasi hicho 54 katika akaunti yake na kuzihamishia akaunti binafsi

Evodia alisema aliyesaidia kupatikana fedha hizo, ni mwanae wa kike ambaye wakati zinaibiwa alikuwa bado mdogo, baada ya miaka sita kupita alipata ufahamu na aliamua kuomba msaada kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagara ambaye baadae aliagiza taasisi taasisi hiyo kufuatilia sakata hilo.

Alisema walifuatilia kwa kina na kugundua fedha hizo ziliibiwa na mtu aliyekuwa amemkopesha mama yake kwa liba miaka sita iliyopita. 

Mkopeshaji riba huyo ambaye hakutajwa jina lake kwa sababu za kiusalama alikiri kufanya hivyo na ndipo ameweza kutoa shilingi milioni kumi za awali na fedha zote zilizobaki atazilipa kila mwezi na kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2020.

Kanali Ndagara alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kufanya semina kwa wafanyakazi wote juu ya tatizo hili la mikopo ya riba linaloendelea kushamiri kila siku kukicha. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles