TAASISI YA NURU KUKABIDHI CHETI KWA JPM

0
1443

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM            |                 


TAASISI ya Nuru ya Taifa imeandaa kongamano la kumpongeza Rais Dk. John Magufuli na kumkabidhi cheti cha heshima kutokana na kazi zake mbalimbali anazozifanya za kujenga taifa.

Kiongozi wa taasisi hiyo, Gadiell Joseph alisema hayo  Dar es Salaam jana kuwa kongamano hilo litafanyika Agosti 31 na linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali   na wasanii.

Alisema  lengo ni kumkabidhi cheti cha heshima na kutukuka kwa kazi ambazo amekuwa akizifanya nchini.

“Hii itakuwa ni tuzo kubwa kuliko tuzo ile ambayo imetolewa na mataifa mengine.

“Sisi vijana tunatambua mchango wa rais katika utendaji wake na ndiyo maana leo tupo hapa tukitembea kifua mbele kutangaza adhima yetu ya kutaka kumzawadia rais siku hiyo,’’alisema Joseph

Alisema Rais Magufuli amekuwa na mchango mkubwa kwa taifa katika kuhakikisha   nchi inakuwa na miundombinu mizuri, kuimarisha usafiri wa anga   na kukua demokrasia nchini.

Februari 17, mwaka huu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alizindua kitabu cha ‘Maajabu ya Rais John Magufuli’ kilichotungwa na Joseph.

Kitabu hicho kilizinduliwa na kusambazwa nchi nzima kwa lengo la kuwafanya watanzania kuelewa zaidi utendaji kazi wa rais ambaye alimwita kuwa lulu ya taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here