KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA

0
732

STELLA SADOCK NaHAPPYNESS GRAYSON-DAR ES SALAAM


MKAZI wa Makumbusho Dar es Salaam, Said Mussa, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kubaka.

Mwendesha Mashtaka, Credo Rugaju alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni,  Anifa Mwingira   kuwa katika tarehe isiyofahamika mwaka huu eneo la Makumbusho, alimbaka binti wa miaka 16 (Jina limehifadhiwa).

Mshtakiwa alikana mashitaka  na alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudushwa rumande hadi  Septemba 4 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Wakati huohuo, mkazi wa Sinza Mori, Mohamed Hamis (24) amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kukutwa na dawa za kulevya.

Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo, Aboud Yusuph alidai  mbele ya Hakimu Mkazi, Boniphace Lihamwike,   kuwa   Januari 10, mwaka huu mshtakiwa alikutwa na  Heroin Hydrochloride yenye uzito wa gramu 0.57.

Mshtakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande hadi    Septemba 3, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here