24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Sumatra yaanza kuwasaka wanaokatisha safari

mziraNA JOHANES RESPICHIUS, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra), imeanza doria ya kukagua na kukamata magari yanayobadilisha njia nyakati za usiku kuanzia saa 10:00 jioni hadi 02:30 usiku.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sumatra, David Mziray, alisema ukaguzi huo utahusisha vituo vyote vya daladala ambapo wataangalia magari yanayobadili njia na nauli inapofika muda wa jioni.

“Sumatra imeanza ukaguzi wa magari yanayobadili njia (ruti) na nauli inapofika jioni na ukaguzi huo utakuwa unaanza saa 10:00 jioni hadi 02:30 usiku katika kila kituo cha kupakilia abiria,” alisema Mziray.

Aidha alisema magari yatakayokamatwa yanabadili njia yatafungiwa au kama dereva hatokuwa na leseni atakata leseni na kulipa faini ya Sh 50,000.

Kutokana na wananchi kulalamika kuhusu mafuta kushuka bei wakati nauli haishuki, Mziray alisema kuwa Sumatra haiwezi kuwa inabadilisha nauli kila mafuta yanaposhuka bali wanaangalia kama yameshuka yatakaa kwa muda gani.

“Haiwezekani tuwe tunashusha nauli kila mafuta yanaposhuka bila kuangalia kama yameshuka na yatakaa kwa muda gani. Je, kama yakishuka mwezi Machi ukashusha nauli halafu yakapanda mwezi wa tano utapandisha nauli tena? Ni usumbufu,” alisema Mziray.

Pia alisema mamlaka hiyo huwa inaweka nauli inayoweza kudumu kwa muda mrefu, akitoa mfano wa nauli iliyowekwa mwaka 2013 ambayo ndiyo inatumika hadi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles