25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

ALAT yataka majipu halmashauri yatumbiliwe

IMG_0046NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shamumoyo amesema baadhi ya halmashauri hapa nchini bado ni majipu zinahitaji kutumbuliwa.

Akizungumza jana Dar es Salaam na waandishi wa habari kuhusu Mkutano Mkuu wa ALAT unaotarajiwa kufanyika Aprili 7 mjini Dodoma, Shamumoyo alisema mfumo wa kielektroniki umesaidia ukusanyaji wa mapato na kuepusha upotevu wa fedha nyingi za Serikali.

“Kulikuwa na mapangufu mengi katika halmashauri zetu ambapo nusu ya halmashauri zilikuwa hazifungi mahesabu na kupata hati chafu, lakini kwa sasa nyingi zimebadilika japokuwa zipo zinazohitaji bado kutumbuliwa kutokana na kutobadilika kwao,” alisema Shamumoyo.

Akitolea mfano wa mabadiliko ya halmashauri na madudu yaliyokuwa yakifanyika hapo awali, alisema Halmashauri ya Kinondoni ilikuwa ikikusanya mapato Sh bilioni tatu hadi kufikia Sh bilioni 48 kwa sasa.

Alisema bado kuna uchafu kwenye halmashauri hapa nchini ni lazima ziendelee kusafishwa ili kufikia malengo tuliyojiwekea.

Shamumoyo alisema kutokana na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato, walilazimika kuanzisha tuzo ambapo halmashauri tano zilishinda, huku Kinondoni ikiibuka mshindi wa jumla wa tuzo za meya na wenyeviti zilizoandaliwa na ALAT mwaka jana.

Alisema kwa sasa halmashauri nyingi zimeweza kujitegemea na kuendesha baadhi ya shughuli za maendeleo kwa mapato ya ndani ambapo wamefanikiwa kujenga maabara tatu katika kila halmashauri na ujenzi wa shule nyingi za Serikali.

Aliongeza kuwa katika mkutano huo watafanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi na kaulimbiu ya mkutano huo ni ‘maboresho ya Serikali za Mitaa kwa utoaji wa huduma bora na maendeleo endelevu’.

Alizitaja nafasi zitakazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti wa ALAT ambaye anachaguliwa na wenyeviti wa halmashauri za wilaya au wenyeviti/mameya wa halmashauri za miji na majiji.

Nafasi nyingine ni makamu mwenyekiti ambaye anachaguliwa na wajumbe wa halmashauri za miji, manispaa na majiji na pia wajumbe wengine watano kutoka kanda tofauti nao watachaguliwa.

Alisema siku hiyo pia watachagua viongozi wa mitandao miwili iliyopo chini ya ALAT ambao ni Mtandao wa Miji (TACINE) na ule wa Mapambano dhidi ya Ukimwi (AMICAAL).

Shamumoyo alisema mkutano huo ambao bajeti yake itakuwa Sh milioni 380, wamefanikiwa kupokea msaada wa Sh milioni 100 kutoka Benki ya NMB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles