Suma Lee kufanya kolabo na Alikiba, Diamond

0
787

 BEATRICE KAIZA 

MSANII aliyekuwa anafanya vema kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva na sasa kuamia kuimba Qaswida Ismail Seif ‘Suma Lee’ ameahidi kfanya kolabo na AliKiba na Diamond Platnumz . 

Akizungumza na MTANZANIA, jana alisema kuwa miongoni mwa mambo anayohitaji kuyatimiza ni kuwaimbisha Qaswida wakali hao wa Bongo Fleva. 

“Nitaimba Qaswida na Diamond na Ali Kiba kwani wote dini yao zinaruhusu iwe kila mmoja na yake au wote kwa pamoja wataimba tu kilazima, kihiari, nitaimba nao,” alisema Suma Lee. 

Aliongezea kwa kuwataka watu kutumia muda wao kwa kumuabudu Mungu kwani kila mtu atafungulia njia yake kwa namna ambavyo anatumia kuwa karibu na wake hata kwenye kipindi iki cha Ramadhani. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here