Misikiti isiyokuwa na vifaa kinga vya corona kufungwa

0
651

Amina Omari, Tanga

Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Tanga limetoa siku tatu kabla haijaifunga misikiti ambayo haitakuwa na vifaa kinga vya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa corona wilayani humo.

Hayo yamesemwa na Shekhe wa Wilaya ya Tanga, Mohamed Kombora leo Jumatatu Mei 4, wakati akizungumza nawaandishi wa habari mkoani Tanga.

Amesema wameanza sambamba na misikiti ambayo imekaidi agizo la kuwataka kuswali kwa kupeana nafasi ya mita moja.

“Tunajua Waislamu si wakaidi tunawaambia wale wanaokaidi watekeleze maagizo ya wataalamu wa afya pamoja na serikali kwa ajili ya maslahi ya jamii yetu kwa ujumla.

“Misikiti ambayo itashindwa kufuata taratibu zilizowekwa ndani ya siku tatu itafungwa ikiwa ni sehemu ya kuwawajibisha kwa kukaidi maelekezo ya serikali na Baraza kwa ujumla,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here