24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Spika Ndugai atishia kutaja wabunge waliotelekeza watoto

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SPIKA wa Bunge Job Ndugai, amesema anayo orodha ya baadhi ya wabunge ambao wametelekeza watoto, hivyo akawataka kila anayehusika na jambo hilo kulimaliza kabla hajawataja.

Ndugai alitoa kauli hiyo   bungeni jana wakati wa kipindi cha maswali na majibu baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Kangi Lugola kujibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Tauhida Galloos (CCM).

Spika Ndugai alisema: “Nakubaliana kabisa na maneno ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwa asilimia mia moja na mimi nishuhudie, ninayo mawasiliano kadhaa ya kina mama kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwalalamikia wabunge wanaume kutelekeza watoto.

“Naomba kila anayehusika na jambo hili achukue hatua ipo siku hapa nitakuja na orodha patakuwa hapatoshi hapa,”alisema Spika Ndugai.

Awali, akijibu swali la Tauhida ambaye alitaka kujua Serikali ina mkakati gani juu ya raia wa kigeni wanaopewa vibali vya kuja kufanya kazi nchini kwa muda na kuwazalisha watoto.

“Pamoja na wadogo zetu na ikifika muda wa kuondoka huwakimbia na kuwaacha watoto wakiishi maisha yao yote bila baba kitu ambacho huwasababishia unyonge katika maisha yao?”aliuliza Tauhida.

Akijibu, Lugola alisema sheria tayari ipo hivyo aliwaomba kina mama ambao wamekimbiwa wafuate sheria.

“Sheria tayari tunayo. Niwaombe kina mama wote ambao wameathirika na jambo hili kwa kuwa ni la jinai waende katika vituo ambavyo vipo jirani wafungue kesi  serikali tutumie kesi hizi kuwarejesha nchini wajibu mashtaka.

“Lakini Mheshimiwa Spika hatua  aliyochukua  Mheshimiwa Makonda ni hatua  lilionyesha dhahiri kwamba siyo wageni tu wanaotelekeza watoto bali isipokuwa hata Watanzania wanatelekeza watoto na tulishuhudia hata hapa ndani sura za watoto zinafanana na baadhi ya watu,”alisema.

Hata hivyo aliwapa ushauri kina mama nchini wazae na  watanzania na kuacha wa nje huku akidai nyumbani kumenoga.

“Nitoe wito kwa kina mama wa Tanzania nawaomba mutumie kilicho ndani ya nchi kilichochenu kuliko kuanza kuliko kutumia raia wa kigeni, rudini humu ndani kumenoga,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles