23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA, NDANDA MZUKA JUU

*Mvua ya saa moja yaairisha mtanange Simba, JKT Tanzania

ZAINAB IDDY- DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga leo kitashuka dimbani Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, kuikabili Ndanda FC, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga itaikabili Ndanda, ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 4 mwaka jana, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga ndio vinara katika msimamo, wakiwa na pointi 67, baada ya kushuka dimbani mara 28, wakishinda michezo 21, sare nne na kupoteza michezo mitatu.

Wapinzani wao katika mchezo wa leo, Ndanda wapo nafasi ya 15 na pointi 36, baada ya kucheza michezo 29, ikishinda tisa, sare tisa na kupoteza mechi 11.

Lakini matokeo ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kati ya timu hizi, unaufanya mchezo huo kutarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kuwa lazima wapate alama 30 katika michezo yao 10 iliyosalia ili kujihakikishia kumaliza ligi kwenye nafasi nzuri.

Zahera aliliambia MTANZANIA jana kuwa, kwa sasa anatengeneza mikakati mizito ya kuhakikisha kikosi chake kinapata matokeo mazuri ili kupunguza kasi ya watu waliopangwa kukikwamisha kikosi chake.

Madai hayo ya Zahera ni mwendelezo wa shutuma zake ambazo amekuwa akirudia mara kwa mara, kwamba kuna mpango wa kuwavuruga katika mbio zao za kuwania ubingwa, lakini wakati huo huo kuzisaidia timu nyingine ziwaondoe katika mbio hizo.

Kocha huyo raia wa DRC alisema: “Kuna watu ndani ya Yanga wanatamani tufungwe kitu ambacho binafsi sikubaliani nacho kwani licha ya hali mbaya ya uchumi tuliyonayo, lakini nimekuwa nikiwahamasisha wachezaji kucheza kwa kujituma.

“Kwa maana hiyo mechi yetu ya kesho (leo), sitarajii kupoteza pointi, kila kitu kwa upande wa Yanga kipo sawa tunasubiri siku na muda ufike ili wachezaji wafanye kazi waliyotumwa,” alisema Zahera.

Zahera ataendelea kujivunia kuendelea kuimarika kwa kiwango cha kiungo wake mahiri Mzimbabwe, Thaban Kamusoko, ambaye alikuwa na mchango mkubwa Yanga ilipoing’oa Alliance na kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Kombe la Azam.

Wakati Zahera akisema hayo, kocha wa Ndanda FC, Khalid Adam, alisema: “Utakuwa mchezo mgumu, Yanga watataka kupata pointi tatu kwetu, lakini haitakuwa rahisi kwa sababu tumejiandaa kikamilifu lakini pia tupo nyumbani,” alisema.

Katika hatua nyingine, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Manispaa ya Morogoro jana, ulilazimika kuahirishwa kutokana na mvua kubwa.

Mvua hiyo iliyonyesha kwa saa moja, kuanzia saa nane hadi saa tisa mchana ilisababisha sehemu ya kuchezea ya uwanja huo kujaa maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles