23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Solskjaer: Nipo tayari kutupiwa lawama

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema yupo tayari kupokea zigo la lawama baada ya juzi kikosi chake kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Newcastle United.

Mchezo huo ulikuwa wa tatu kupoteza kwa Manchester United tangu kuanza kwa msimu huu huku wakishinda michezo miwili na kutoa sare michezo mitatu na kuwafanya washike nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo nane.

Kichapo hicho cha juzi Manchester United walikipokea huku wakiwa hawana baadhi ya mastaa wao uwanjani kama vile Paul Pogba na Anthony Martial, hivyo wakashindwa kutamba kwenye uwanja wa St. James Park.

Kutokana na hali hiyo, Solskjaer amekuweka wazi kuwa, yupo tayari kutupiwa lawama kutokana na mwenendo wa timu hiyo, lakini anaamini mambo yatakuja kubadilika.

“Hakuna ambaye anafurahia mwenendo wa timu kwa sasa, najua kwenye mchezo huo dhidi ya Newcastle tuliwakosa baadhi ya wachezaji wangu, lakini hicho sio kigezo.

“Ninaamini wachezaji wangu walipambana sana lakini mwisho wa siku tunajikuta tukiwa sehemu ambayo hakuna aliyefikiria kama tungeweza kuwepo. Naweza kusema hatukuweza kutengeneza nafasi za kutosha kwa ajili ya kushinda mchezo huo.

“Tumekuwa pamoja kama timu lakini tumeshindwa kuutawala mchezo na kupata matokeo mazuri,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo kocha huyo aliongeza kwa kusema, kuna wakati wachezaji wake walionekana kama wametoka mapumziko ya timu za taifa.

“Kuna wakati wachezaji wangu walikuwa wanaonekana kama wametoka kwenye mapumziko ya timu za taifa, lakini lazima tuangalia nini kimetokea kwenye michezo yote nane ambayo tumecheza.

“Hakuna wa kulaumiwa mwingine ni mimi mwenyewe wa kutupiwa lawama, ninatakiwa kuhakikisha ninalimaliza tatizo hili. Kuna wachezaji wamekosa uzoefu, lakini ninaamini muda mfupi wale ambao wapo majeruhi watakuwa fiti na kuisaidia timu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles