24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Soko la madini lazinduliwa Same

Safina Sarwatt,Same,

Serikali mkoani Kilimanjaro imezidua soko la  kuuza   madini aina ya Metali na vito wilayani Same, kutokana na wilaya hiyo kuongoza kuwa na madini mengi kuliko wilaya zote za mkoani humo.

Wilaya zingine ambazo zimegundulika kuwa na madini kama hayo ni Mwanga, Rombo, Siha na Moshi Vijijini.

Akizungumza wakati alipokuwa akifungua soko hilo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Anna Mghwira amesema soko hilo litakuwa likifanyika  mara mbili kwa mwezi lengo ni kukuza soko la madini na kuongeza thamani .

Amesema soko hilo litaisaidia serikali kukusanya mapato sahihi yatokanayo na madini pamoja na kudhibithi utoroshaji wa madini lakini pia litasaidia kujua viwango vya uzalishaji madini aina Metali na Vito katika wilaya Same na kukusanya mapato sahihi.

“Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini  kutorosha  madini na kuikosesha serikali mapato hivyo kuanzishwa kwa soko hili  katika wilaya hii litasaidia kudhibiti utoroshaji wa madini,”amesema.

Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka sita mwaka tangu mwaka 2014 hadi kufikia mwaka huu sekta ya madini mkoani Kilimanjaro imeweza kuchangia mapato ya jumla ya Sh.936, 510, 303.19.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles