29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Anayedaiwa kumuua mwanafunzi wa Kampala mikononi mwa polisi

Leonard Mang’oha-Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ernest Joseph (19) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Mgaya aliyefariki dunia Juni 17 baada ya kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Juni 19, Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Madale jijini hapa.

“Mtuhumiwa katika mahojiano na Jeshi la Polisi amekiri kumchoma kisu kilichosababisha  kifo cha mwanafunzi huyo huku akieleza namna mwanafunzi huyo alivyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio kuwa ni TSHIRT nyeusi,suruali ya Jinsi na Kapelo nyeusi.

“Aidha mtuhumiwa alikiri kumpora pochi iliyokuwa na simu moja aina ya Tecno rangi nyeusi,  fedha taslimu Sh 8,000 na vitambulisho mbalimbali ambavyo alivitupa na simu hiyo kuiuza,”amesema.

Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mambosasa pia amedai kuwa jeshi hilo linawashikilia watu 31 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uporaji katika maeneo ya vyuo mbalimbali jijini hapa.

“Wanafunzi wa vyuo vikuu vyote Dar es Salaam wawe na amani tumeanza msako mkali na niwaambie wale wanaojihusisha na vitendo hivi wajiepushe hawatabaki salama” amesema Mambosasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles