22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Chama cha wauguzi chasikitishwa na Serikali kushusha alama za ufaulu

Asha Bani -Dar es Salaam  

Chama cha wauguzi nchini (TANNA)kimesikitishwa na hatua ya serikali ya kushusha alama za kujiunga na vyuo kutoka alama C mbili na D moja  hadi D tatu jambo ambalo wamesema kinashusha ubora wa taaluma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Juni 19, Rais wa chama hicho,  Paul Magesa amesema kitendo cha wizara kushusha alama hizo kutafanya kupatikana wauguzi wasio na ubora na kuhatarisha maisha ya Watanzania.

“Serikali imetangaza kushusha alama za kujiunga fani ya  uuguzi kutoka ya awali iliyokuwa ikihitajika yaani Fizikia, Kemia na Biolojia kupata alama C, C, D na sasa D, D, D jambo ambalo litasababisha kuwa na wauguzi wasio na ubora na ni hatari.

“Sisi chama hatukubaliani wala kuafiki uamuzi huo wa wizara ambao unalenga kushusha ubora wa taaluma ya uuguzi na huduma zitolewazo na wauguzi nchini ambazo zinahitajika umahiri mkubwa,”amesema Magesa.

Aliongeza kuwa wanapenda kuona viwango vya elimu ya uuguzi vikiboreshwa zaidi ili kupata wauguzi wenye wenye weledi wa hali ya juu kama ilivyokwisha kuanishwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga nchini na sababu zilizotolewa na serikali kushusha alama hizo ni ukosefu wa wanafunzi katika vyuo binafsi jambo ambalo si sahihi na wala njia bora.

“Sisi tumegundua sababu mbalimbali ni kwamba vyuo binafsi vina ada kubwa na michango mingi na wapo wanafunzi wengi wenye alama za juu lakini vyuo vya afya ni vichache.

“Lakini pia chama cha wauguzi tunapenda kuhoji hawa wenye alama dDD watatumia mtaala upi wakati mtaala uliopo ni wenye udahili CCD kwa maana ya maudhui yaliyomo zinalenga watu wa aina hii ya ufaulu wa CCD kuwa ndio watakaoweza kujifunza na kuelewa hatimaye kuwa na wauguzi wazuri,”amesema Magesa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles