23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

India yaipatia Tanzania Dola za Marekani milioni 500 kuboresha miradi ya maji

Serikali  imesema imepata fedha kutoka Serikali ya India kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 500 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya maji  kwa miji 28 ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.

Hayo yameelezwa leo Juni 19, bungeni na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema).

Katika swali lake, Lijualikali alidai kwamba mtandao wa maji katika Mji wa Ifakara ni asilimia 40 ya mahitaji yake.

“Je,Serikali ina mapango gani wa kuongeza mtandao huo,”aliuliza Lijualikali.

Akijibu swali hilo, Aweso amesema kwa mpango wa muda mrefu, Serikali imepata fedha kutoka Serikali ya India kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 500 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya maji  kwa miji 28 ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.

Amesema kwamba Mji wa Ifakara ni miongoni mwa miji ambayo itakayopata maji kupitia fedha hizo.

Aweso amesema mpango wa muda mfupi Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) imekamilisha mradi  wa uboreshaji wa huduma za maji katika Mji huo.

“Kazi zilizokamilika katika mradi huo ni ujenzi wa nyumba za pampu, ufungaji wa pampu mbili na ujenzi wa mtandao wa bomba kilometa 8.4,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles