29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Sitta apinga magari ya Tanzania kuzuiwa Kenya

NA samwel-sittaABRAHAM GWANDU, ARUSHA
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ameshtushwa na hatua ya Serikali ya Kenya kuyazuia magari yenye namba za usajili za Tanzania kuingia katika eneo la maegesho ya magari katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata na kuweka wazi kuwa ni hatua isiyokubalika.
Akizungumza kwa njia ya simu na MTANZANIA jana, Sitta alisema hatarajii kama hatua hizo zina baraka za uongozi wa Serikali ya Kenya, huku akiwatupia lawama watendaji wa ngazi za chini nchini humo.
“Ni vitendo ambavyo havikubaliki ,si sawa kabisa na vitaiangamiza Jumuiya ya Afrika Mashariki hatukubali hata kidogo, kuna mengi yanayotokea huko dhidi ya masilahi ya Tanzania na kwa kweli vinaweza kuiua jumuiya,”alisema Sitta.
Alisema Serikali ya Tanzania itachukua hatua haraka kufuatilia jambo hilo na itawasilian na viongozi wakuu wa Kenya ili kunusuru hali hiyo iliyosababisha mtafaruku na usumbufu kwa wageni ambao wengi ni watalii.
“Mimi na waziri mwenzangu wa jumuia upande wa Kenya tunatambua msimamo wa Rais wa Kenya kuhusu jumuia lakini nina shaka na watendaji wa chini katika Serikali na mamlaka kadhaa za Kenya zinaweza kuleta matatizo makubwa katika muungano wetu,” alisema Sitta.
Alitoa mfano wa shirika la viwango la nchi hiyo kukataa kununua mahindi ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo kwa madai kuwa yana sumu wakati mahindi hayo hayo yanaingizwa Kenya kupitia nji za panya.
Wakizungumzia usumbufu huo katika eneo la Astro lilipo geti la kwanza la kuingia uwanjani hapa madereva wanaowapeleka watalii katika uwanja huo kutoka kampuni mbalimbali za kitalii walisema hatua hiyo imewapa adha kubwa wageni hasa watalii.
Ruben Kiondo dereva wa Kampuni ya Rainbow Shuttle, alisema anashangazwa na kitendo cha usumbufu wanaoendelea kupata hasa watalii wanaokuja nchini Tanzania, huku Serikali ikikaa kimya.
“Huwezi kuamini lugha isiyo nzuri wanayojibiwa watalii wanaoelekea Tanzania kupitia uwanja huu wakihoji askari wanaozuia magari ya Tanzania kuingia uwanjani, mara wanaambiwa kwa nini msipande ndege huko uwanja wa Kilimanjaro, tutawazuia msipite hata mpaka wa Namanga,” alisema Kiondo.
Mfanyabiashara kutoka Arusha ambaye naye alifika katika lango la kuingilia uwaanjani hapoa juzi akiwa na gari dogo lenye namba za usajiliza Tanzania Patel Bhatia alisema kuwa alifika katika uwanja huo kwa lengo la kuwachukua ndugu zake kutoka Uingereza lakini alizuiwa kuingia na kukaa nje hadi alipowasiliana na ndugu zake.
“Huu ni ustaarabu gani? kwanza wageni wangu waliwasili kwa kutumia ndege ya shirika la Kenya kuna sababu gani ya kuzuiwa nisiingie na gari binafsi kuwachukua,”alihoji Bhatia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles