22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Simulizi: Baba wa wake 16, watoto 151

AMA hakika, mkazi huyo wa Wilaya ya Mbire iliyoko Jimbo la Mashonaland, Zimbabwe, ameuamua kuutendea haki ule mstari wa kwenye maandiko matakatifu ya Biblia, pale tulipoambiwa ‘Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki…’

Akiwa na umri wa miaka 66 kwa sasa, Misheck Nyandoro, ni mume wa wanawake 16, ambao kwa pamoja ‘wamemjazia nchi’ kwa kumzalia jumla ya watoto 151.

Pasi na shaka swali la msingi unaloweza kuwa nalo ni je, Nyandoro anafanya kazi gani ya kumwezesha kuihudumia familia kubwa kiasi hicho?

Jibu ni kwamba wala hana kazi ya kumwingizia kipato na badala yake anatumia muda mwingi kufanya ngono na wake zake ili kuwaridhisha.

Tegemeo lake kubwa kiuchumi ni watoto wake, ambao wengi wao sasa ni wakubwa na wanafanya kazi za kuwaingizia kipato cha kumsaidia mzee wao.

Ingawa 50 bado wanasoma, wapo wanaojihusiaha na kilmo, sita ni wanajeshi, wawili ni polisi, 11 wameajiriwa katika taaluma mbalimbali, wakati mabinti zake 13 wameshaolewa.

“Watoto wangu wananiokoa. Mara nyingib huwa napokea zawadi na fedha kutoka kwao na hata kwa wajukuu zangu,” anasema mzee huyo akihojiwa na gazeti la The Herald la Zimbabwe.

“Kwa siku, kila mke wangu anapika na kuniletea chakula. Lakini sharti ni moja tu, nitakula kile ambacho ni kitamu sana.”

Aidha, mmoja kati ya watoto wake anaonekana kufuata nyayo za mzee kwani tayari ameoa wanawake wanne.

Juu ya anavyoweza ‘kukata kiu’ ya kila mmoja wao, Nyandoro anasema huwa anahakikisha anawazungukia wake wanne kila usiku mmoja.

“Huwa nakwenda kwenye chumba ambacho ratiba inanionesha na nikishamridhisha mke wangu, basi nahamia chumba kingine. Hii ndiyo kazi yangu. Sina kazi nyingine,” anasisitiza.

Kama ulidhani familia kubwa hiyo ni mzigo kwake, basi utakuwa unakosea sana. Unajua kwanini?

Nyandoro anatarajia kuoa mke wa 17 katika siku zijazo, ndoto yake ikiwa ni kuhakikisha wanafikia 100.

Kwa upande wa watoto, yeye anatamani kuona wanafikia 1 000 kabla hajaondoka duniani.

Cha kufurahisha, anasema kwa sasa anataka kuoa wanawake ‘wabichi’ kwani wale wenye umri mkubwa wameshindwa kwenda na kasi yake ya kufanya ngono.

Nyandoro alianza utamaduni huo wa kuoa wake wengi mwaka 1983 na anasema hajawahi kuona mke wake yeyote akiwa hafurahii maisha ya ndoa yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,283FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles