28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yakiuka agizo la TFF

messi1NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Klabu ya Simba umekiuka agizo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuwataka wafanye mazungumzo mapya na mchezaji wao, Ramadhani Singano ‘Messi’, kwa madai kuwa amekwenda kinyume cha makubaliano yao kwa kutoa siri juu ya kilichozungumzwa kwenye kikao hicho.
Maamuzi hayo ya Simba yalitolewa jana kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, kilichokaa juzi kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo, ikiwemo sakata la mchezaji wao huyo.
TFF iliagiza Simba na mchezaji huyo kufuta mikataba yote na kuingia kwenye makubaliano mapya kwa ajili ya msimu mpya wa 2015/2016.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema Messi amevunja makubaliano kwa kuvujisha siri za kikao hicho walichokaa kati yake, uongozi wa Simba, Chama cha Wacheza Soka Tanzania (SPUTANZA) na TFF, ambapo walikubaliana kwa pamoja kutotoa siri ya mazungumzo yao.
“Kwakuwa Messi alivunja makubaliano yaliyoamuliwa kwa pamoja katika kikao hicho ya kutozungumzia yaliyojadiliwa na kupendekezwa kwenye vyombo vya habari, Klabu ya Simba imeamua kutokufanya mazungumzo na mchezaji huyo hadi pale mkataba wake utakapofikia ukomo Julai mosi, mwakani.
“Amesema yeye ni mchezaji huru, amekiuka makubaliano yetu, Simba itakuwa tayari tena kufanya naye mazungumzo baada ya mkataba huo kukamilika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mkataba,” alisema Aveva.
Alieleza kuwa wanatarajia mchezaji huyo ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia upo TFF na kwenye mtandao wa TMS.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles