26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Usaili BSS mikoa minne

Madam-RitaNA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM
MSIMU wa tisa wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba, maarufu kama ‘Bongo Star Search’ unatarajia kuanza rasmi mwezi ujao, ambapo kwa mwaka huu usaili utafanyika katika mikoa minne tu.
Akizungumza jijini jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo, Rita Paulsen, alisema mwaka huu watafanya usaili katika mikoa minne, baada ya kufanya uchunguzi na kugundua washiriki wanajirudia katika mikoa yote.
“Mwaka huu usaili tutaufanya katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam, kila mtu mwenye kipaji atapaswa kufika kwenye mikoa tuliyoitaja na tumepanga kuchagua washiriki watano watano kutoka kila mkoa isipokuwa hapa jijini,” alisema Rita.
Alisema tarehe ya usaili ni Julai 4 hadi 26, ambapo hapa jijini amepanga kuchagua washiriki 15.
Alisema mashindano hayo yataonyeshwa katika vituo vya televisheni vya Clouds Tv na Star Tv, ambao ni miongoni mwa wadhamini.
Kwa upande wa Meneja wa Masoko wa Kampuni ya PSI ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo, Gaston Shao, alisema wamelenga kuibua vipaji na kuhakikisha wasanii wanajilinda kiafya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles