MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unatarajia kutaja majina ya wanachama wake watakaokabidhiwa nyumba 13 katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa mtandao huo, Cassim Twaalib, alisema mkutano huo utafanyika katika ofisi zake zilizopo Ilala, Bungoni Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi.
Twaalib aliongeza kwamba pia watatangazwa viongozi watakaoshika nafasi za uongozi zilizo wazi ambazo ni Makamu Mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Marehemu Kepteni Komba, Katibu ambayo ilikuwa inashikiliwa na Selemani Pembe ambaye yupo India kikazi na Mweka Hazina, Flowin Nyoni, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa sasa.