29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Miss Albino kupatikana leo usiku

ISHA MASHAUZIIIINA GEORGE KAYALA

KUNDI la Mashauzi Classic Modern Taarab linatarajiwa kutoa burudani kali ya kukonga nyoyo za mashabiki watakaoshuhudia shindano la kumsaka mrembo wa watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Miss Albino’, linalofanyika katika Ukumbi wa Msasani Club, jijini Dar es Salaam leo usiku.

Tamasha hilo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation (SVF) kupitia Baraza la Sanaa nchini (Basata).

Mratibu wa tamasha hilo, Fredy Kaula, ambaye pia ni Mwenyekiti wa shirika hilo, alisema awali walipanga kuwa na Christian Bella, lakini katika hatua za mwisho walishindwa kumpata kutokana na mambo yalivyokuwa juu ya uwezo wao, lakini watakuwa na wasanii wengine, wakiongozwa na Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic.

 

Kaula aliongeza kwamba tamasha hilo linalenga kuibua na kutambua vipaji, kujenga ujasiri, kuwawezesha kufikia malengo yao, kuwajenga kiafya, kiuchumi na kielimu pia.

“Pia katika shindano hilo tunatarajia kupata Sh milioni 90 ili zisaidie ujenzi wa maktaba na jiko katika kituo cha walemavu kilichopo Buhangija, Mkoa wa Shinyanga,’’ alisema Fatuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles