Diamond awafunika wakali 15 wa Afrika

0
1019

diamond-numzNA HERIETH FAUSTINE

MKALI wa wimbo wa ‘Nana’, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, ameshika nafasi ya kwanza katika orodha ya waandaaji wa tuzo ya African Music Magazine (Afrimma), iliyowataja wasanii 15 waliofanya vizuri kutoka Afrika kwa mwaka huu.

Kupitia tovuti ya Afrimma, Diamond ameshika nafasi ya kwanza akifuatiwa na msanii kutoka Nigeria, Wizkid, nafasi ya tatu imechukuliwa na Olamide huku ya nne ikienda kwa Davido, wote kutoka Nigeria.

Imeelezwa kwamba orodha hiyo imetokana na Diamond kunyakua tuzo tatu za Afrimma, ikiwemo ya mwanamuziki bora wa mwaka, katika mashindano yaliyofanyika Dallas, Marekani, Oktoba 10, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here