BAADA ya kushambuliwa kwa maneno na mashabiki wake wakihitaji video ya wimbo wake wa ‘Subira’, msanii mahiri nchini, Kassim Mganga, leo anatarajiwa kuiachia video hiyo ili kupoza mashabiki wake hao.
Wimbo wa ‘Subira’ ambao Kassim amemshirikisha mkali wa sauti, Christian Bella, unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini bila ya kuwa na video yake.
“Muda mrefu nimekuwa na kigugumizi juu ya maswali ya mashabiki wangu kuhusu video ya wimbo wa Subira, lakini sasa nimeshaukamilisha na kesho ‘leo’ nauweka hadharani,
“Sikuwa na sababu yoyote ya kukurupuka kuachia video hii kwa kuwa nilikuwa nahitaji video nzuri na yenye kiwango cha juu machoni mwa mashabiki wangu,” alifafanua Kassim.