26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Shirika lazindua kampeni kutokomeza magonjwa ya kuambukiza

Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

SHIRIKA la WaterAid Tanzania, limezindua kampeni ya ‘usichukulie poa, unategemewa’, yenye lengo la kuboresha tabia za usafi miongoni mwa jamii ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza ikiwamo corona.

Kampeni hiyo yenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya watu wake kupitia kuimarika kwa tabia kunawa mikono ili kuimarisha usafi nchini, imefadhiliwa na Unilever na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID).

Mkurugenzi Mkazi wa WaterAid, Anna Mzinga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana

kabla ya kuzindua kampeni hiyo, alisema licha ya kuwapo udhibiti mkubwa wa mamabukizi ya corona bado ugonjwa huo upo na kwamba wana jukumu la kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuepuka magonjwa mengine ya kuambukiza kupitia kampeni hiyo.

Alisema kampeni hiyo iliyozinduliwa jana imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwamo mchezaji wa mpira wa miguu, Juma Kaseja na msanii wa mashairi Mrisho Mpoto kwa ajili ya kutoa elimu jamii katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita na Zanzibar.

“Kampeni hii itaendelea hadi Januari na itahusisha kusambaza na kueneza ujumbe wa mabadiliko ya tabia ya usafi kupitia vyombo vya habari pamoja na matukio ya ushiriki wa jamii,” alisema Mzinga.

Alisema ili kusaidia wananchi kubadili tabia, kampeni hiyo itahusisha pia ujenzi wa vifaa vya kunawia mikono kwenye vituo kadhaa katika maeneo yenye shughuli nyingi na yenye watu katika maeneo manne yaliyolengwa.

Mzinga alisema wanatarajia kusambaza jumla ya vifaa saba vya kunawia mikono katika maeneo manne ya Dar es Salaam na kila kifaa kimoja kina uw- ezo wa kutumiwa na watu 5,280.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Abdallah Mtinika, aliitaka kampeni hiyo kuwafikia wananchi katika mitaa mbalimbali na wanafunzi mashuleni.

Alisema makundi hayo yakifikiwa ni wazi kuwa jamii itaelimika na kujenga mazingira ya kupenda usafi wa mazingira wakati wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles