25.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

Walioshinda kura za maoni CCM kikaangoni

CHRISTINA GAULUHANGA NA FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, amesema watawashikisha adabu walioshinda kura za maoni ndani ya chama hicho kwa kukiuka maadili na makatazo ya chama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Polepole alisema, chama hicho kinaendelea na vikao vya uteuzi kwa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge huku wakiwa wamepokea lundo la malalamiko katika ofisi yao.

Alisema kwa wagombea waliofuata sheria waendelee kuwa watulivu na kwa wale waliokiuka maadili katika chaguzi za kura za maoni watawafundisha adabu.

“Wagombea waliofuata maadili mkae mtulie mambo yanaendelea, kwa wale wenzetu waliokiuka maadili mwaka huu mtajionea surprise tutawashikisha adabu,’’alisema Polepole.

Alisema wale wachache ambao wamejaribu kutoa rushwa watashangaza kwakuwa mwaka 2016 mkutano Mkuu wa chama hicho na ule wa halmashauri ulifanya mageuzi ya kiuongozi, kioganizesheni na kiutendaji ambao ulikubaliana kupata viongozi wanaochukizwa na rushwa.

Akizungumzia kuhusu mchakato uchaguzi ndani ya chama kwa ngazi zote, alisema umekwenda vizuri na dunia nzima imeshangazwa jinsi kulivyokuwanauwazinademokrasia.

“Kwa sasa tunaendelea na vikao vya mapendekezo na rai yangu endeleeni kuwa watulivu na malalamiko yanaruhusiwa kutolewa katika ofisi zote za chama, tunazo taarifa nyingi na katika kipindi hiki kwa wanaodhani biashara ni kama kawaida tutawashangaza,”alisema Polepole.

Polepole alisema kwa mujibu wa sense waliyoifanya baada ya ugonjwa wa Covid 19 kuisha, wana mtaji wa wapiga kura milioni 16.8 ambao ni wana- chama hai wa chama hicho.

“ Tuna mtaji wa kura hizi hadi sasa hapo bado mambo mazuri yaliyofanywa na Rais. Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu na tuna asilimia 68 ya vijana wanaotuunga mkono,” alisema Polepole.

WIMBO WA TAIFA

Katika hatua nyingine Polepole alisema chama hicho kimesikitishwa na kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuongeza ubeti wa tatu wa katika wimbo wa taifa.

Alisema kitendo cha Chadema kufanya hivyo, kimemuumiza yeye pamoja na Watanzania kwani hata CCM inazo nyimbo nyingi haijawahi kuubadili Wimbo wa Taifa.

Aliwasihi Chadema inatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo walichokifanya japokuwa wao wanadai hakuna sheria inayokataza lakini kuna makubaliano kuwa ni nembo za taifa.

“Kwa jinsi ambavyo nawajua Chadema kamwe hawataweza kuwaomba radhi Watanzania, baada ya chama hicho kubadili ubeti wa wimbo wa taifa na kuufanya kuwa wa chama chao.

“Chadema iwaombe radhi Watanzania ila mimi najua hawataomba radhi, kama mnabisha tubet hapa, ni desturi yao, nimefanya nao chaguzi nyingi wanavunja sheria, juzi wamemsema vibaya kila mtu kwenye nchi hii, chama hiki ni tatizo kubwa “ alisema Polepole.

Kuzindua nyimbo za kampeni

Katika hatua nyingine Polepole alisema chama hicho kinatarajia kufanya tamasha kubwa la kuzindua nyimbo zitakazotumika katika kabla ya kampeni, wakati wa kampeni na nyimbo za kushangilia ushindi.

Alisema tayari nyimbo hizo zimetungwa na wasanii 109 wakiwamo wakubwa wanaotamba ndani na nje nchi pamoja bendi za muziki.

Aliwataja wasanii hao kuwa ni Naseeb Abdul (Diamond) na wasafi, Ali Kiba na kundi lake, Hamonize, Peter Msechu na bendi nyingine kama Twanga pepeta, TOT PLUS na nyinginezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,649FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles