28.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

TPDC yatoa elimu ya usalama wa gesi asilia Mtwara

Na Mwandishi Wetu-Mtwara

SHIRIKA  la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) limezindua semina ya utoaji elimu ya nyumba kwa nyumba kuhusu usalama na matumizi ya gesi asilia kwa watumiaji majumbani kwa wateja wapya waliounganishwa na nishati hiyo asilia.

Akizungumza leo mkoani Mtwara katika kampeni hiyo ya elimu ambayo inatarajiwa kuendeshwa pia katika Mikoa ya Lindi, Pwani na Dar es Salaam, Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma kutoka TPDC, Delian Kabwogi amesema kampeni hiyo inalenga kuwafikia watumiaji wa gesi asilia wa majumbani  na Taasisi.

Amesema wanatarajia kutembelea nyumba 425 na Taasisi ambazo tayari zimeunganishwa na mtandao wa utumiaji wa gesi asilia. 

“Elimu hii ni endelevu na inalenga kuendelea kuwakumbusha watumiaji wa gesi asilia na Watanzania kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kuitunza miundombinu ya gesi asilia lakini pia suala la usalama na vitu gani vya kiuzingatia pindi suala la dharura linapojitokeza wakati wa kutumia gesi asilia,” amesema  Delian.

Aidha, Delian  ameongeza kuwa, TPDC ililazimika kusitisha matumizi ya gesi asilia kwa watumiaji wote wa Mkoa wa Mtwara ili kukamilisha taratibu za kiusalama kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watumiaji pamoja na miundo mbinu inakuwa salama muda wote wa matumizi. 

“Gesi  asilia kwa uasili wake haina harufu hivyo kufanya utambuzi wake pindi inapovuja kuwa mgumu, TPDC kwa kulitambua hili lilifanya utaratibu wa kuagiza kemikali maalumu ambayo inapaswa kuchanganywa katika gesi asilia ili kuipa harufu ambayo mtumiaji anaweza kutambua kwa urahisi pindi hitilafu inapoteka kuna kuvuja kwa gesi hiyo. 

“Kemikali hii tayari imekwishafika Mtwara ambapo ilikuwa imechelewa kuingizwa hapa nchini baada ya janga la Corona ambalo liliibuka  mwishoni mwa mwaka 2019 na kuathiri sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa bidhaa kutoka nje na ndani ya nchi,” ameongeza Kabwogi.

Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara, wameipongeza hatua hiyo kwa kusema kwamba itasaidia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza gharama za nishati pamoja na kuepusha uharibifu wa mazingira ambao unatokea kutokana na ukatajai wa miti kwa ajili ya kuni pamoja na uchomaji mkaa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,637FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles