24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Shetta aingia kwa ubabe shoo ya Juma Nature

SHETANA RHOBI CHACHA

AKIWA na wapambe 15 msanii wa Bongo Fleva, Nurdin Bilali ‘Shetta’, alilazimika kutumia nguvu za ziada ili kuingia na wapambe wake hao katika shoo ya kuadhimisha miaka 16 ya muziki kwa msanii Juma Nature, iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

Shetta ilimlazimu kufanya uamuzi huo baada ya njia yake ya kutishia kususia kufanya onyesho lake katika onyesho hilo kupuuzwa huku akikataliwa kuingia na idadi hiyo kubwa ya wapambe wake badala yake alitakiwa aingie na wapambe nane tu.

Kabla ya Shetta kutumia nguvu, wapambe wake nane waliokubaliwa kuingia ukumbini walimtaka msanii wao huyo waondoke kama wenzao hawatakubaliwa kuingia huku wakilalamika kwamba mbona msani Nassib Abdul ‘Diamond’ huwa na wapambe wengi lakini hawawazuii.

“Hapa kwa vile Shetta mnamzuia lakini angekuwa Diamond angeingia na wapambe wake hata ishirini na msingemzuia kwanini Shetta bora tusepe,” alipaza sauti mmoja wa wapambe hao.

Hata hivyo, Shetta alipohojiwa alishangazwa na kukataliwa wakati huwa anaongozana na wapambe 15 katika kila onyesho lake, lakini hata hivyo onyesho lilifanyika kwa mafanikio na Nature akafurahia miaka yake 16 huku kituo cha EFM kikisherehekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles