25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Cheka amtwanga Mthailand, kuzichapa na Muiran

NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka, juzi aliibuka kidedea kwa kumtwanga Mthailand, Kiatchai Singwancha kwa TKO (Technical Knock Out) raundi ya nane.
Mara baada ya ushindi huo, Cheka atapanda tena ulingoni mwishoni mwa Julai mwaka huu kupambana na Sajjad Mehrabi raia wa Iran.
Katika pambao hilo la raundi 10 (Kg 79) lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, Cheka alimdhibiti mpinzani wake huyo ambaye aliumia mkono raundi ya nane na kushindwa kuendelea na pambano hilo na Cheka kupata ushindi wa TKO.
Akizungumza na MTANZANIA mara baada ya ushindi wake, Cheka alisema ushindi huo umetokana na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimpa sapoti hali iliyopelekea kuweza kufanya vizuri.
“Namshukuru Mungu kwa ushindi huu vile vile na mashabiki wangu ambao wamekuwa wakinipa sapoti kubwa, kilichobaki ni kujipanga katika pambano linalokuja dhidi ya bondia wa Iran. Nitaendelea kujifua vema ili kurudisha ubora wangu,” alisema.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Antony Lutta, alisema kutokana na ushindi huo, Cheka atapigana na bondia huyo raia wa Iran, pambano litakalofanyika nchini mara baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
“Hii itakuwa kwa mara ya pili Cheka kuzidunda na Sajjad, katika pambano la mara ya kwanza lililofanyika mwaka jana walitoka sare, hivyo tumeona turudie tena ili tuone nani mbabe kati yao,” alisema.
Matokeo ya mapambano ya utangulizi yaliyolipamba pambano hilo, ilishuhudiwa Shaaban Kaoneka akimpiga Zumba Kukwe kwa pointi, Twaha Kiduku naye alimtwanga Seleman Zugo kwa pointi, huku Epson John akimchakaza Shedrack Juma kwa pointi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles