26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Snura akwepa ‘viroba’ stejini

snura1NA RHOBI CHACHA

KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii wa filamu na muziki, Snura Mushi, alijikuta akirushiwa pombe zilizokuwa katika vifuko vidogo maarufu viroba akiwa jukwaani kama njia ya kumshangilia kwa uchezaji wake.

Snura alipanda jukwaani na kuimba wimbo wake ulioshika chati nchini wa ‘Nimevurugwa’ katika onyesho la miaka 16 ya msanii Juma Nature lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini.

Snura akiwa jukwaani, shabiki mmoja alimfuata na kumtunza kiroba kisha idadi nyingine ya mashabiki ikaendelea kumtunza fedha pamoja na viroba hivyo.

Hata hivyo, msanii huyo alionyesha upendo kwa mashabiki hao kwa kuwarushia zile pombe za viroba alizotunzwa huku fedha alizotunzwa akiziweka mfukoni.

Zawadi nyingine aliyoitoa Snura baada kutunzwa fedha na viroba alikuwa akikatika kiuno chake kwa mashabiki waliokuwa wakimtunza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles